YEE PROGRAM
10/1/2025
RECAP || YEE PROGRAM, YOMBO –Siku ya mwisho ya Mafunzo iliwakutanisha wasichana waliopata watoto katika umri mdogo kutoka kata ya Kiwalani Mtaa wa Yombo.
Wasichana hao waliweza kupata mafunzo ya ujasiriamali na uelewa wa mikopo ya asilimia 10 kutoka halmashauri.
Wakiwa chini ya mwongozo wa wataalamu kutoka sekta mbalimbali, walipata nafasi ya kujifunza mbinu mbalimbali za kujitegemea kiuchumi, kuunda vikundi vyao, na kujadili fursa zilizopo katika jamii yao.