Youth Empowerment with Mulika

10/1/2025

Shukrani za dhati kwa wasichana wenye watoto katika umri mdogo kutoka kata za Kibaigwa, Mlali na Chiwe waliojitokeza kushiriki mafunzo ya Youth Economic Empowerment (YEE) wilayani Kongwa.

Kupitia mafunzo haya, walipata nafasi ya kujifunza stadi za kiuchumi, kuunda vikundi vya pamoja, na kuelekezwa kuhusu fursa za mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri. Ushirikiano na ari waliyoonyesha ni mfano wa kujitolea na dhamira ya kujiletea maendeleo.